Monday, July 18, 2011

SARAKASI BUNGENi!!!

Wabunge kutoka chama tawala na upinzani wameonyesha dhahiri shahiri kuwa wanaisimamia serikali pale (kwa ukali kabisa) walipoituhumu wizara ya Nishati na Madini inayoongozwa na William Ngeleja kwa matumizi mabaya ya fedha za wananchi na hivyo Kiranja mkuu (Pinda) kulazimika kuomba muda wa wiki tatu zaidi ili serikali ijipange vizuri.Pinda ameonyesha hasira kali kwa Katibu mkuu wa wizara hiyo(hadi kufikia kutamka kuwa angekuwa na mamlaka ya kumfukuza ngetamani kumfukuza mara moja) aliyeagiza idara zilizo chini ya wizara hiyo kuandaa milioni hamsini kwa kuwa bajeti imeshapita katika kamati ya Bunge ya Nishati na madini.Huu ni ukomavu na utashi wa hali ya juu wa kisiasa!